Mtume paulo wa kwenye Biblia alisema asiyeyanya kazi na asile.Wengi tunafnya kazi je tunapata tunachotahili?
Haya mawazo yamenijia baada ya kufuatilia mwenedo wa bunge la katiba na kiasi cha posho wanachopata ambacho wao wanaona hakitoshi.
Tujiulize maswali yafuatayo
Je ni wajumbe wangapi wamechagia tangua kuanza kwa bunge hili maalum na je ni wangapi hawajachangia?
Je ni wajumbe wangapi wamekuwa wazomeaji na je ni wangapi wamekuwa wakitekaleza wajibu wao?
Je ni wangapi wamekuwa kikwazo kwa mwendo mzima wa semina tangu zianze?
Je ni wabunge wangapi wamekuwa wakitetea maslahi ya vyama vyao na kusahau maslahi ya taifa?
Je kwa mwenenndo huu wa bunge hili tutapata katiba liyo bora kwa maslahi ya taifa?
Baada ya kujiuliza maswali hayotujiulize mengine pia
Je adi sasa bunge hili maalum la katiba linatimiza wajibu wake ipasayo?
Na mwisho kabisa tujiulize je wanastahili posho wanazopewa ama WANAKULA BURE BILA KUFANYA KAZI?
No comments:
Post a Comment