Video link hapo juu ni revi2w ya ujumbe wa Video ambao Papa Francis amewatumia Waprotestant na Wapentekosti.
Ili uone uzito wa ujumbe huo, nimetoa utangulizi kidogo sana wa kiunabii.
UNABII WA DANIEL NA UFUNUO
Ukisoma Mathayo 24:15, Yesu anasema, "ukiona chukizo la uharibifu, lile lililonenwa na nabii Daniel, limesimama katika patakatifu (asomaye na afahamu).
Mstari wa 20, Ombeni ili kukimbia kwenu kusiwe wakati wa baridi, wala siku ya sabato, 21, Kwa kuwa wakati huo kutakuwapo dhiki kubwa...
Daniel
1. Anatoa unabii wa matukio ya siku za mwisho. Unabii huo unahusisha falme kuu 4 ambazo zilitawala ulimwengu, yaani Babel, Uamedi na Uajemi, Uyunani (Greece) na Rumi.
2. Kuhusu Rumi. Daniel 7:23-26
"Akanena hivi, huyo mnyama wa nne atakuwa ni ufalme wa nne juu ya dunia...25 Naye atanena maneno kinyume chake Aliye juu, naye atawadhoofisha watakatifu wake aliye juu, naye ataazimu kubadili majira na sheria; nao watatiwa mikononi mwake kwa wakati [siku 360], na nyakati mbili [360 x 2 =720] na nusu wakati [1/2 × 360 = 180] [jumla ni siku 1260].
Ona maajabu ya Mungu. kuhusu siku 1260 Yohana katika Ufunuo anandika, Ufunuo 13:5 - Naye akapewa kinywa cha kunena maneno makuu, ya makufuru. Akapewa uweza wa kufanya kazi yake kwa miezi 42 [42 x 30 (siku za mwezi) = 1260].
Ufunuo 12:6 [hapa hesabu inaandikwa kwa maneno kabisa] Yule mwanamke akakimbilia nyikani, ambapo ana mahali palipotengenezwa na Mungu, ili wamlishe huko muda wa siku elfu na miambili na sitini [1260]. [Katika kipindi cha mateso yaliyotekelezwa na Rumi kanisa la kweli la Mungu lilihifadhiwa]
UMUHIMU WA SIKU 1260
1. Hizo ni siku za kiunabii, yaani siku moja sawa na mwaka mmoja (Ezekiel 4:5-6, ...siku moja kwa mwaka mmoja). Kwahiyo siku 126o ni sawa na miaka 1260
2. Miaka 1260 ilianza mwaka 538 mwaka ambao Rumi ya Kikristo ilianza kutawala na ikaishia mwaka 1798. Ilipokamilika miaka 1260 ya unabii, Papa Pius wa VI alichukuliwa mateka na Jemedari wa Kifaransa Berthier.
3. Je yaliyotabiriwa kwaajili ya miaka 1260 katika Daniel 7:25 yalitimia:
● Kubadili majira na sheria je?
● Kumwaga damu ya watakatifu je? Kanisa liliua maelfu ya watu waliopingana na madundisho yake. Baadhi yao ni John Huss, Jerome n.k. Mwaka 2005 Papa John Paul II aliomba msamaha kwa niaba ya kanisa. Ufunuo 17:6 anaandika, Nikamwona yule mwanamke [Kanisa] amelewa kwa damu ya watakatifu na kwa damu ya mashahidi wa Yesu...
4. Katika kipindi cha miaka 1260 ndio walitokea Waprotestant mfano, Martin Luther, Tindale na John Huss. Leo wanaitwa Waprotestant kutokana na kupinga au kuprotest dhidi ya mafundisho ya Kanisa Katoliki yaliyo kinyume na biblia.
RUMI SEHEMU YA PILI
Baada ya anguko la Rumi mwaka 1798, Yohana anaona katika unabii Kanisa tena likishamiri. Yohana anaandika.
Ufunuo 13:1-4
"3 Nikaona moja cha vichwa vyake kama kwa kimetiwa jeraha la mauti [tukio la mwaka 1798] na pigo lake la mauti likapona. Dunia yote ikamstaajabia myama yule [Papa anachukuliwaje na Dunia ya leo eg. USA, UK etc?].
Upapa [Rumi] Unajipanga kufanya nini?
1. Ufunuo 13:7 - Tena akapewa kufanya vita na watakatifu na kuwashinda, akapewa uwezo juu ya kila kabila na jamaa na lugha na taifa.
2. Ukisoma Ufunuo 13:11 utaona jinsi Marekani inavyotabiriwa kuisaidia Rumi kukamilisha adhima yake. Unadhani itashindakana? Muulize Mseven kinachompata kwaajili ya sheria ya ushoga. Ukitafakari hilo soma Ufunuo 13:17. Vikwazo vya kiuchumi! It is possible.
PAPA ANATAKA NINI
1. Anatoa wito kwa Waprotestant na Wapentekosti kurudi Rumi. Katika utangulizi anajinasibu kwa kusema Uprotestanti ulikwisha???
2. Anataka madhehebu yaungane. Kwanini yaungane wakati mambo waliyoyakimbia Waprotestant kwakumwaga damu bado yapo Rumi.
Wito wa tumaini
Ufunuo 14:7 - akasema kwa sauti kuu, mcheni Mungu na Kumtuza kwa maana saa ya hukumu yake imekuja. Msujudieni yeye aliyezifanya mbingu na nchi na bahari na chemichemi za maji.
ONYO
Soma Ufunuo 14:8-14
Sasa angalia wito wa Papa kwa kubofya hapahttps://www.youtube.com/watch?v=7kgxEvIDoGs
Ukiwa na swali nishilikishe.
Asante kwa kusoma
MUNGU akubariki
Wapendwa nilianza makusudi kwa kuandika Mathayo 24 : 15 Heri asomaye na afahamu...
Wapendwa nilianza makusudi kwa kuandika Mathayo 24 : 15 Heri asomaye na afahamu...
Ili muelewe vizuri kwani Papa anatoa wito kwa Waprotestant na Wapentekosti kuungana na Kanisa la Romani Catholic. Ni lazima uelewe unabii wa kitabu cha Daniel na Ufunuo.
Nilichofanya hapo nikutoa high level summary ili kuwachokoza msome zaidi.
Janeti nilikwisha mpatie kitabu kilichoandika habari hizi kwa undani lakini naye anasema hajaelewa.
Mungu anataka habari hii ihubiriwe kwa kila mtu ili kama unaamua kuingia katika muungano haramu wa makanisa upotee kwa kutaka mwenyewe. Wito huu upo katika Ufunuo 14.
Kupata Resources zaidi download android app inaitwa EG White estate. Utapata zaidi ya vitabu na machapisho 50.
Search kitabu kinaitwa the Great Controversy.
Please read, it is for your eternal salvation or loss. It is important you make an informed decision.
Kwa mtakao anza kusoma. Key ya unabii hii hapa:
Kwa mtakao anza kusoma. Key ya unabii hii hapa:
Joka - shetani
Mwanamke - kanisa
Kahaba - kanisa linalochanganya mfundisho ya mabwana wawili yaani ya Yesu na ya Shetani
Mnyama - taifa au ufalme
Pembe - taifa au nchi
Siku - mwaka
Maji mengu - watu wengi
Nchi kavu - maana yake watu wachache
Chapa ya mnyama / alama ya mnyama/ sanamu ya mnyama - 666 au Sunday worship as oppossed to Sabbath
Mwanamke - kanisa
Kahaba - kanisa linalochanganya mfundisho ya mabwana wawili yaani ya Yesu na ya Shetani
Mnyama - taifa au ufalme
Pembe - taifa au nchi
Siku - mwaka
Maji mengu - watu wengi
Nchi kavu - maana yake watu wachache
Chapa ya mnyama / alama ya mnyama/ sanamu ya mnyama - 666 au Sunday worship as oppossed to Sabbath
Madini eg. Dhahabu, Fedha, Shaba, Chuma - Falme
Ukikutana na kitu huelewi nijulishe.
Anza na Ufunuo 13 na 14
Enjoy your reading
No comments:
Post a Comment