- A. CHIMBUKO LA MAFUNDISHO YA IMANI YA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO
1) Je Waadventista Wasabato ni akina nani? Je wametokeaje? Je wana utume gani?
2) Kama vile ambavyo Yohana Mbatizaji aliuelewa utume wake kwa kusoma Maandiko ya Nabii Isaya, (Yohana 1:19-26), ndivyo Waadventista Wasabato nao walivyotakiwa kuuelewa utume wao kwa kusoma Maandiko ili yafunue utume wao umejengwa juu ya nini.
3) Kwa kuyasoma Maandiko, Kanisa la Waadventista Wasabato limejitambua kuwa ni,“Kanisa la Masalio la Unabii wa Biblia”. Utambulisho huu umejengwa juu ya unabii wa Ufunuo sura ya 12. Ni taasisi ya kidini iliyoanza baada ya siku 1260 au miezi 42 ya mateso ya Kanisa lililokimbilia nyikani, (Ufunuo 12:1-6; 13-17; Ufunuo 13:1-7).
4) Baada ya kipindi cha mateso ya kanisa kwisha, masalio (walioamua kutokumuasi maagizo ya Mungu), walitambulika kwa kutetea amri za Mungu na kuwa na ushuhuda wa Yesu, (Ufunuo 12:17). Ushuhuda wa Yesu ni mafunuo ya utimilifu wa unabii uliotolewa na Yesu kuhusu hali ya kanisa lake itakavyokuwa kipindi baada ya kipindi na waumini waliomo ndani wanavyotakiwa kutenda katika kipindi husika, (Ufunuo 1:1,2; Ufunuo 19:10).
5) Utume wa Kanisa la Waadventista Wasabato umejengwa juu ya ujumbe wa malaika watatu wa Ufunuo 14:6-12; uwanja wa utume ni kukabiliana na mamlaka inayoshindana na Mungu na Kanisa inayoelezwa katika Ufunuo 13.
6) Utume wa Kanisa unaotajwa katika Ufunuo 14:6-12 umegawanywa katika makundi matatu:
a) Ujumbe wa Malaika wa Kwanza
i. Kumtambulisha Mungu na madai yake kwa wanadamu walio chini ya utisho wa mamlaka inayompinga Mungu, watu wa kila taifa na kabila na lugha na jamaa,(Ufunuo 12:6; Ufunuo 13:1-8), ili wajulishwe uwezo na mamlaka ya Mungu juu yao.
ii. Kumweleza mwanadamu: chimbuko lake na uhitaji wake iii. Kulieleza tatizo la dhambi na suluhisho lake, (Wokovu)
iv. Kuelezea kicho cha Mungu kilivyo
v. Wito wa kumcha na kumwabudu Mungu,(Kanisa la Mungu lilivyo) vi. Kutangaza kuwadia kwa saa ya hukumu ya Mungu na haja ya kujisalimisha kwa Mungu, (Mambo ya siku za mwisho).
b) Ujumbe wa Malaika wa Pili
i. Kumtambulisha mpinzani wa Mungu na utendaji wake
ii. Kufichua udanganyifu wa mpinzani wa Mungu kimwenendo na kimafundisho, kwa kuuleza ukweli wa Mungu uliopotoshwa na mpinzani. (Maisha na Mwenendo wa Mkristo).
c) Ujumbe wa Malaika wa Tatu
i. Wito kwa wanadamu kumwabudu Mungu peke yake
ii. Maonyo kwa wanadamu watakaomtii mpinzani wa Mungu
iii. Kutangaza hukumu ya Mungu kwa walioamua kumuasi Mungu na kumtii mpinzani wake
7) Ni kutokana na ujumbe wa hawa malaika watatu, kanisa la Waadventista limezalisha mafundisho 6 yenye misingi 28 ya Imani ifundishwayo katika kipindi hiki.1. Fundisho kuhusu Mungu- Misingi -5
a) Maandiko Matakatifu
b) Utatu Mtakatifu
c) Mungu Baba
d) Mungu Mwana
e) Mungu Roho Mtakatifu
2. Fundisho kuhusu Mwanadamu- Misingi -2
a) Uumbaji
b) Asili ya Mwanadamu
3. Fundisho kuhusu Wokovu- Misingi -4
a) Pambano Kuu (Baina ya Kristo na Shetani)
b) Maisha, Mauti, na Ufufuo wa Kristo
c) Uzoefu wa Wokovu
d) Kukua katika Kristo
4. Fundisho kuhusu Kanisa – Misingi -7
a) Kanisa (katika upana wake)
b) Masalio na Utume wake
c) Umoja katika mwili wa Kristo
d) Ubatizo
e) Meza ya Bwana
f) Karama za Roho na Utume
g) Karama ya Unabii
5. Fundisho kuhusu Maisha ya Kikristo yalivyo- Misingi -5
a) Sheria ya Mungu
b) Sabato
c) Uwakili
d) Mwenendo wa Mkristo
e) Ndoa na Familia
6. Fundisho kuhusu Mambo ya Siku za Mwisho- Misingi- 5
a) Huduma ya Kristo katika Hekalu la mbinguni
b) Kuja kwa Kristo mara ya pili
c) Mauti na Ufufuo
d) Milenia (Miaka Elfu) na mwisho wa dhambi
e) Dunia mpya
Misingi 8 kati ya hii misingi 28 hudhihirisha utofauti wetu na madhehebu mengine kiimani na kimafundisho. Hii ni pamoja na: Masalio na Utume wake; Karama ya Unabii; Sheria ya Mungu; Sabato; Huduma ya Kristo Katika Hekalu la Mbinguni; Kuja kwa Yesu Mara ya pili; Mauti na Ufufuo; na Milenia (Miaka elfu na mwisho wa dhambi).
1(e).Roho MtakatifuMungu Roho wa milele alikuwa mtendaji pamoja na Baba na Mwana katika uumbaji, kufanyika mwili, na katika ukombozi. Aliwavuvia waandishi wa mabadiliko matakatifu. Alijaza maisha ya Kristo na uwezo. Huwavuta na kuwasadikisha wanadamu, na wale wanaoitikia huwafanya upya na kuwabadilisha katika sura ya Mungu. Akipelekwa na Baba na Mwana ili kuwa siku zote pamoja na watoto wake, hutoa karama za kiroho kwa kanisa, huliwezesha kumshuhudia kristo, na kwa upatano wa maandiko uliongoza kwenye ukweli wote. (Mwa 1,2. Luka 1:35, 4:18. Mdo 10:38. 2Petr 1:21. 2Wakor 3:18. Yoh 14:16-18,26, 15:26,27, 16:7-13
Nimeipenda
ReplyDeleteMzuriiii sana
ReplyDeleteGood lesson specifically event of the destiny
ReplyDeleteAmen
ReplyDeleteNi nzuri sana
ReplyDelete