27 April 2014

MIAKA 50 YA MUUNGANO

Ni tukio la kujivunia sana na la kumshukuru sana Mungu alietuunganisha na kutufanya wamoja kwa mda wa nusu karne. Jana tumeshehekea miaka hamsini tangu kuzaliwa kwa taifa la Tanzania baada ya mataifa ya Tanganyika na Zanzibar kuungana mwaka 1964. Ni sherehe ambazo zimefana sana na ni sherehe za aina yake ambapo tulishushudia maonesho ya uwezo wa jeshi la wananchi baada ya miaka hamsin ya muungano.
Mengi yalisemwa na mengi tuliyashhudia kwa macho na mengi yametukia hasa siku za karibun ndani ya bunge maalum la katiba.
Binafsi nawapongeza watanzania wenzangu kwa hatua tulofikia japo sina nia ya kumchosha yeyote kwa lolote wote tutafakari ni kipi knatokea saivi? je ni kweli tume ya katiba na rasim yake wana nia ya kuuvunja muungano? je ni kweli UKAWA wana nia ya kuuvunja muungano? Je ccm ndo wana nia ya dhati ya kuulinda Muungano?
Maisha ya ajabu sana kwa binadam maana hata chizi anajiona ni mzma kuliko mtu yeyote yule. Hii ndo hatari sana kwa mustakabali wa nchi kwayale nloyaona bungeni pamoja na matamko mbalimbali pamoja na hotuba ya raisi alipokuwa anawahutuba vijana wa ccm! hapa napata shaka kama kweli nia ni kuuinda muungano ama ni kukomoana kisiasa!
JUMAPILI NJEMA

No comments:

Post a Comment