09 April 2014

NAFASI ZA KAZI TANAPA

Mhifadhi Wanyamapori Daraja La II – (NAFASI 10)

Nafasi hizi ni kwa ajili ya Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii.


MAJUKUMU YA KAZI
    Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi
    Kudhibiti vitendo vya ujangili nje na ndani ya hifadhi
    kusimamia uwindaji wa kitalii na utalii wa picha
    kulinda Nyara za Serikali
    Kusimamia usafirishaji wa wanyamapori na nyara nje na ndani ya Nchi
    Kusimamia matumizi ya magari ya doria
    Kukagua wanyamapori kwenye mashamba na mazizi ya wanyamapori na kutunza takwimu zao
    Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba
    Kudhibiti moto katika hifadhi
    Kukusanya na kutunza vielelezo vya ushahidi na kutoa ushahidi Mahakamani
    Kukusanya takwimu za wanyama na mimea kwenye hifadhi
    Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa zinazoendana na taaluma yake


SIFA ZA MWOMBAJI

    Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au kidato cha VI wenye Stashahada ya Uhifadhi Wanyamapori (Diploma in Wildlife Management) kutoka Chuo cha Usimamizi Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.


MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGS C kwa mwezi.

Masharti Ya Jumla Kwa Kazi Zote.

i. Waombaji wote wawe ni Raia wa Tanzania.
ii. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
iii. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi za kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
iv. Nafasi ya kazi inayoombwa iandikwe katika kichwa cha habari cha barua na juu
ya bahasha, kutozingatiwa hili kutasababisha maombi ya kazi kuwa batili.
v. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu za kuaminika pamoja na majina ya wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
vi. Maombi yote yaambatane na vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika. Viambatanisho hivyo vibanwe sawa sawa kuondoa uwezekano wa kudondoka au kupotea.

- Shahada ya juu/Shahada/Stashahada ya juu/Stashahada/Astashahada.
- Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI
- Cheti cha Kompyuta
- Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards)
- Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni iandikwe jina kwa nyuma.

vii. “Transcripts”, “Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.

viii. Waombaji wawe na umri usiozidi miaka 45.
ix. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika utumishi wa umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
xi. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kupokea barua za maombi ni tarehe 15 Aprili, 2014
xiii. Aidha, uwasilishaji wa barua kwa mkono katika ofisi za Sekretarieti ya Ajira HAURUHUSIWI.
xiv. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU na NECTA).
xv. Maombi yanaweza kuandikwa kwa Lugha ya Kiswahili au Kiingereza na yatumwe kupitia posta kwa anuani ifuatayo;-

Katibu,
Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma,
SLP.63100,
Dar es Salaam.

AU

Secretary,
Public Service Recruitment Secretariat,
P.O.Box 63100
Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment